Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014, akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.
Zitto akizungumza na wanafunzi
Wanafunzi wakipiga makofi, wakati mwenyekiti huyo akizungumza nao
Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014.Picha na K-Vis Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Shule yangu ya zamani bado inadai. Hapo kama 7C njia ya kwenda staff. Mwandishi ameshindwa hata kupata jina la mwalimu mkuu?

    ReplyDelete
  2. Kama walengwa wamefikiwa na hiyo chenji hilo ni jambo zuri..

    ReplyDelete
  3. Sasa Chenji ya Rada mnakwenda Shule ya Bunge Dar nendeni Shule za Kisiju ama Ubena Zomozi mkaone !

    Achilia CHENJI YA RADA YA JESHI huko mwanawane hata ile CHENJI YA BUNDUKI GOBORE hawaioni kwenye Sekta ya Elimu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...