Tungependa kukukaribisha kwenye huduma yetu ya Usafiri jijini kwa kutumia mabasi maalumu kwa sababu kuu tatu au zaidi.
1. Tunaamini wafanyakazi wanaotumia muda mrefu njiani kwa kutafuta usafiri, au kwa kukwama kwenye foleni wakati wakielekea makazini, huwa wanafika wamechoka tayari na hivyo kupelekea kuwa na umakini wa kiwango cha chini pamoja na kupunguza uzalishaji.
2. Kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakati ukiendesha gari, inaaminika kuwa ni mazingira yanayosababisha kiwango cha juu sana cha msongo, na ni sababu ya watu wengi kutokuwa na furaha kwa muda mwingi wawapo makazini.
3.Gharama za kuendesha gari kwa siku moja kwenye jiji la Dar es Salaam, kwenda kazini na kurudi zinakisiwa kuwa zaidi ya Tsh. 30,000/= kwa gari ya kawaida yenye viti vitano. Hii inamaana kuwa kwa kila kiti kimoja cha gari lako, kinakugharimu Tsh. 6000/=. Endapo unatumia kiti kimoja tu cha gari lako, inamaanisha unapoteza Tsh. 24,000/= kwa kila siku unapotumia gari lako kwenda kazini, kwa siku 20 za kazi ni sawa na Tsh. 480,000/= na ni zaidi ya Tsh. 5,760,000/= kwa mwaka zinazopotea kwa wewe kuendelea kutumia gari lako binafsi kwenda kazini na kurudi.
Kampuni ya City Ridez Travels & Tours ingependa kukuletea suluhisho la matatizo haya kwa ujumla wake. Lengo letu ni kupunguza idadi ya magari binafsi yanayotembea muda wa kwenda na kurudi kazini kwa kukuletea usafiri maalumu, wenye starehe, wakutegemewa na kwa gharama nafuu.
Hapa City Ridez Travels & Tours tunahusika na usafiri maalumu wa mabasi, kwa minajili ya kutoa njia mbadala ya kusafiri ukiwa ndani jiji. Kimsingi tukizingatia zaidi kwenye Ubora, Uaminifu na Usalama.HABARI ZADI BOFYA HAPA.
Sijawaeleweni!
ReplyDeleteHapa UK hiyo inaitwa "Car Share" ni kuwa mwenye gari anachukua abiria ambao watachangia harama za mafuta. Hii mara nyingi una-share na watu unaokwenda nao sehemu moja. Pia gari za binafsi zenye abiria zaidi ya mmoja zinaruhusiwa kupita katika "Bus Lane". Hii ni sera ya serikali ya UK kupunguza misongamano ya magari.
ReplyDelete