Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, George Liundi wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho

 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu George Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa kweli picha ya mwisho, wazee wote wameshika videvu inatia huzuni sana, nafikiri wanatafakari mustakabali wa kila mwanaadam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...