Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Bashir Mrindoko akieleza namna anavyo kasirishwa na mwenendo wa kusuasua kwa baadhi ya miradi ya maji nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Kigoma, ASaimon Lupuga aliyesimama nyuma akijibu swali la Katibu Mkuu namna wakandarasi wanavyotekeleza miradi ya maji mjini Kigoma, wengine ni baadhi ya maafisa wa Wizara, wakuu wa mamlaka za maji, wakandarasi na wakandarasi washauri.

Na Athumani Shariff,

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Bashir Mrindoko amelazimika kukutana na wakandarasi na wakandarasi washauri wanaotekeleza baadhi ya miradi ya maji nchi nzima Ubungo Maji Makao Makuu ya Wizara ya Maji jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho pia kiliwahusisha wakurugenzi wote wa Wizara ya Maji, kilikuwa na lengo lakutathini mwenendo wa miradi ya maji nchini na kuangalia namna ya kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika kikao hicho Katibu Mkuu hakufurahishwa na namna ambavyo wakandarasi wengi wanavyofanya kazi polepole huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kero ya kukosa huduma ya maji.

“Si ridhiki na namna munavyofanya kazi haswa wakandarasi wa miradi ya Morogoro, nataka muangalie namana ambavyo munaweza kufanya ili mukamilishe miradi hiyo kwa wakati” alisisitiza Mrindoko.

Aidha alisema hatosita kukatisha mikataba na wakandarasi wazembe na wale ambao wanachelewesha miradi kwa visingizio visivyo vya msingi.

“Hapa juzi tu nimekatisha mkataba na mkandarasi wa mradi wa maji wa Chalinze, hivyo kwa yoyote atakayezembea sitoacha kumkatishia mkataba, na atake haribu kazi nitamshitaki katika bodi ya wakandarasi ambayo na mimi mwenyewe ni mjumbe” aliongezea Katibu Mkuu.

Baada ya maelezo yake mafupi, Katibu Mkuu aliwasimamisha wakandarasi washauri katika kila mradi kueleza namna miradi wanayoisimamia inavyotekelezwa na kisha kuwanyanyua wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kueleza jinsi wanavyotekeleza na kuweka ahadi lini wataikamilisha.

Wakieleza katika kikao hicho, baadhi ya wakandarasi wamejitetea kuwa miradi mingi ya maji imekuwa ikichelewa kutokana na changamoto mbalimbali, vikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi, malighafi, ucheweshwaji wa bidhaa bandarini, ukosefu wa umeme wa uhakika, taratibu za TRA na upatikanaji wa mabomba viwandani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...