Kiongozi wa msafara wa Kifimbo cha Malkia kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Kipchoge Keino (kulia) akimkabidhi Kifimbo cha Malkia kwa Mkuu wa msafara kwa Tanzania Gullam Rashid mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo ambaye pia aliwakilisha Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika mapokezi ya Kifimbo cha Malkia Bi. Juliana Yassoda (katikati) akipokea Kifimbo hicho kutoka kwa Mke wa Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania Bi. Anna Bayi leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dianna Patricia Melrose akiwa na Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi (mwenye miwani) wakiwa na watoto waliofika uwanja wa ndege kupokea Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi akiwa katika picha na vikundi vya ngoma vilivyotumbuiza wakati wa mapokezi ya Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hatareee!!!!

    ReplyDelete
  2. Hiki kifimbo kina significance gani kwa Mtanzania wa leo? Neo-colonialism in its workings!!! Wajinga ndio waliwao!

    ReplyDelete
  3. Hichi kifimbo kinatusaidiaje sisi?

    ReplyDelete
  4. Nasie wa Sweden na Scandinavia tunakisubiri hiko kifimbo...kije Sweden kipokelewe na Malkia na mfalme wa huku...sio mfaidi nyie tu na hiko kifimbo.....Ama kweli bado tupo gizani, yaani kama mtu anaamua kukutumia fimbo kama kiwakilishi chake nasi kukipokea kifimbo na kuserebuka nacho kwa namna hii...sioni hajabu na jinsi tunavyooingizwa kingi na kupigwa changa la macho kila uchao.

    ReplyDelete
  5. Na kifimbo cha mchonga wamekipeleka kuwaonyesha waingereza?

    ReplyDelete
  6. Bora kifimbo cha malkia kuliko cha mfalme

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...