Kiongozi wa msafara wa Kifimbo cha Malkia kwa Ukanda wa Afrika Mashariki Kipchoge Keino (kulia) akimkabidhi Kifimbo cha Malkia kwa Mkuu wa msafara kwa Tanzania Gullam Rashid mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo ambaye pia aliwakilisha Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika mapokezi ya Kifimbo cha Malkia Bi. Juliana Yassoda (katikati) akipokea Kifimbo hicho kutoka kwa Mke wa Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania Bi. Anna Bayi leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dianna Patricia Melrose akiwa na Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi (mwenye miwani) wakiwa na watoto waliofika uwanja wa ndege kupokea Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) Filbert Bayi akiwa katika picha na vikundi vya ngoma vilivyotumbuiza wakati wa mapokezi ya Kifimbo cha Malkia leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari.







Hatareee!!!!
ReplyDeleteHiki kifimbo kina significance gani kwa Mtanzania wa leo? Neo-colonialism in its workings!!! Wajinga ndio waliwao!
ReplyDeleteHichi kifimbo kinatusaidiaje sisi?
ReplyDeleteNasie wa Sweden na Scandinavia tunakisubiri hiko kifimbo...kije Sweden kipokelewe na Malkia na mfalme wa huku...sio mfaidi nyie tu na hiko kifimbo.....Ama kweli bado tupo gizani, yaani kama mtu anaamua kukutumia fimbo kama kiwakilishi chake nasi kukipokea kifimbo na kuserebuka nacho kwa namna hii...sioni hajabu na jinsi tunavyooingizwa kingi na kupigwa changa la macho kila uchao.
ReplyDeleteNa kifimbo cha mchonga wamekipeleka kuwaonyesha waingereza?
ReplyDeleteBora kifimbo cha malkia kuliko cha mfalme
ReplyDelete