Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. KAZI IPO KIJIWENI,TUKIWA NA WATU KAMA HAWA WAWILI TUU KIJIWE KITAKAMILIKA.

    ReplyDelete
  2. benja yaani umenichekesha sana nikweli kama mtu una uraia wa nchi unayoishi basi usitake uraia mwingine baki na huohuo la uukane huo ulio nao upewe unaotaka big up benja.hilo lipo sawa wanataka uku na uku tamaa zao mbaya.

    ReplyDelete
  3. Kwa mtu mwenye kuchangia maendeleo ya taifa mama lake hatakuwa na mawazo finyu. Wanaotaka uraia pacha si kwa faida yao wao,la hasha! Ni kusaidia vizazi vyetu vilivyobaki huko ili wapate unafuu wa shida za kila siku. Mimi ni mdau wa ughaibuni,kupata services muhimu za mahitaji ya binadamu,chakula,mavazi,malazi, ni rahisi,ongezea elimu ya bure. Matibabu nayo. Sasa nikisikia babu,bibi,mjomba,shangazi wa kule kijijini shida kupata au vipo lakini quality sio nzuri,huwa inaamsha hisia za kibinadamu kuwa tufanye nini kuboresha haya mambo. Na kikwazo kikubwa cha kuwekeza kuinua maisha ya watz wenzetu ni hii hali ya wasiwasi kuwa ukimuudhi kiongozi wa kijiji basi ataweza kutaifisha vilivyo vyakp kisa sheria ya uraia haikuruhusu kumiliki vitu kadhaa.

    ReplyDelete
  4. Nafikiri wabunge na mawaziri wetu hawatilii maanani suala la uraia wa nchi mbili haswa upande wa mtanazania.Mfano ambao ni wa ukweli ni kama wazungu na wachina amabao wamekuja na kukaa hapa wanaoa mwanamke wa kitanzania na kupewa uraia wa Tanzania bila ya wao kuambiwa wa ukane uraia wa kwao.kitu wanachokita wao ni kupata ardhi na mali asili.angalia waisrael walivyooa wamasai arusha na sasa kumiliki mashamba ya kahawa.Uraia wa taifa mbili hauna tatizo lolote kwa mmzawa.Hawa watanzania wenzetu wenye asili ya asia wote wana uraia wa taifa kibao lakini hakuna mtu yoyote anayewakalia kooni.

    ReplyDelete
  5. Jamaa huyo mwenye miwani(Nadhani anaitwa (Mwambapa) kelele nyingi jamani. Na ni kweli ni CCM, hajui kushindama kwa hoja. Wenzako wanasema kwamba Uraia pacha una faida kama 1. watoto wao kuwa raia wa TZ baadaye na kurithi migomba(ardhi), 2. Mataifa mengi na sana yaliyopo karibu na TZ wote wana uraia pacha, wametaja Kenya na Uganda, 3. Watanzania Diaspora wanapenda kuwa wa TZ sababu ya maisha ndiyo yanawafanya wawe na uraia pacha. Yeye anasema ohooo!! "sijui mnataka kuwa na uraia pacha ili muwe wabunge halafu mkitibua mkimbilie Marekani, (samahani wana CCM, kweli jamaa wote walioko Ughaibuniwanaweza kuwa wabunge?!!). Samahani tena, mie sina chama Bongo lakini kweli sasa naanza kuamini akili ndogo imetawala akili kubwa Bongo kwa mdua sasa. Kwa mawazo kama haya. Jamaa na safari yote ya Marekani na kusoma kote anaongea pumba. Afadhali angekaa kimya, kwani hapa anajizalilisha. Ndiyo maana nasemaga vyama TZ ni sifuli, wangeacha tu mgombea binafsi. Halafu jamaa muoga kama nini,(mie Mnyakyusa wa Tukuyu lakini sijawi ona Mnyakyusa muoga kama jamaa hapa) waache wenzio waandamane, wakufanyie kazi wewe halafu ufaidi matunda ya damu yao baadaye, sindiyo zenu wabongo. Lakini kuongea, anaongea kama kameza radio Pumba kabisa.

    ReplyDelete
  6. Bwana Mwaipaja kumbe ni mtu wa busara sana. Leo kathibitisha busara zake katika mjadala huu. Sababu hasa inayowafanya Watanzania waishio nchi za nje kupewa uraia mbili ni nini hasa? Mtu kama ulishaukana Utanzania na sasa unautaka tena kwanini usiukane uraia wa nje uliopewa na kurudi kuwa raia wa Tanzania? Kuna ubaya gani?
    Kwa upande wa viongozi wa Tanzania nawauliza hivi? Enzi za Mwl. Nyerere Watanzania waliokuwa wakisoma ama kuishi nje ya Tanzania, walikuwa wakiteuliwa kuwa Wakurugenzi au kupewa kazi muhimu katika serikali ya Tanzania wakiwa huko huko nchi walizokuwa wakiishi. Kulitumika vigezo gani hadi mtu kupata nafasi kama hizo? Mbona baada ya Nyerere kuondoka hatujasikia uteuzi wa aina hiyo? Je, hamuoni kuwa ilikuwa ni motisha kubwa kwa Watanzania waishio nje kuipenda zaidi nchi yao na kutaka kubaki kuwa Watanzania na matumaini makubwa ya kuthaminiwa Utanzania wao?

    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  7. Hoja si kutafuta ubunge,wengi wanaoutaka uraia pacha wana kazi zao zinazolipa sanaaa,kurudi bongo kufanya kazi hatuwezi kuwa-afford. Ila ujuzi wao ni hazina kwa taifa. We need them more than they need us. Thats the reality. Watz tubadilike,twendeni na wakati. Nafikiri mzee Benja anaongelea makada wenzake ambao kutwa tunawaona wanakimbizana na viongozi bongo kutafuta vyeo bila elimu na huko ughaibuni maisha yamewapiga chenga,hawana namna,ni utapeli kwa kwenda mbele na kujitangaza kwenye fb,mablogs etc. Hapa nawakilisha watu wenye career zao na vyeo vyao ughaibuni ambao hawahitaji kukwaa vyeo bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...