Na Mwandishi Wetu, Moshi

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo (TLP), Dk. Augustino Mrema, amezindua mashindano ya soka, Mrema Cup 2014, yatakayoshirikisha jumla ya vilabu 15 kutoka katika kata zote 15 ya jimbo hilo.

Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya uzinduzi huo, Dk. Mrema alisema lengo la mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika jimboni hapo ni kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta mshikamano katika jamii.

Dk. Mrema alisema kwa sasa hakuna sekta inayofanya vizuri katika kutoa ajira kwa vijana kama michezo huku akisistiza umuhimu wa kushiriki michezo kwa lengo la kuhamasisha Amani, mshikamano na umoja katika jamii.

“Tunazindua mashindano haya kwa lengo moja tu, kuhamasisha mshikamano, amani na udugu wetu, dunia nzima hakuna sekta inayochangia kutoa fursa za ajira kama michezo hasa mchezo wa soka, vijana wakishiriki michezo wanapata kazi lakini pia inasaidia kuimarisha Afya,” alisema Dk. Mrema

Naye, Mratibu wa Mashindano hayo, inspecta msaidizi wa polisi kituo cha himo, Laban Sospeter alisema, Vilabu vitakavyoshiriki katika mashindano hayo ni Himo, Njia panda, Kahe, Makomu, Mamba, Kilema, Mandaka, Riata, Makuyuni, Mitsubishi na Kifaru ambayo ni timu mwalikwa.

Laban alisema baada ya uzinduzi huo, wanatarajia kuanza mashindano hayo wiki ijayo ambapo katika mechi ya uzinduzi kati ya Njia panda FC na Himo SC ulishuhudia Njia panda wakiibuka na ushindi wa 1-0.

Zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili ni shilingi laki tatu na mshindi wa tatu akiondoka na laki mbili fedha taslim ambapo jumla ya shilingi milioni moja zita zitashindaniwa.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014, katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikagua wachezaji wa klabu ya Himo na Njia panda katika mechi ya uzinduzi wa Mrema Cup 2014, uliofanyika juzi katika viwanja vya Himo, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014, katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duh! Mhe. inaonekana anaumwa. Hopefully ana take care kisukari chake vizuri. Piga kazi mzee.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahim sana kumuona Mzee Lyatonga Mrema baada ya miaka kadhaa hivi.

    Lakini nina wasiwasi hivi Mzee Augustino tungali tupo wote TLP ama mwenzetu umesha tupa Jongoo na mti wake umerudi CCM?

    Ni kwa rangi za pamba ulizopiga kwa kuwa nina amini Wapinzani wengi kama wana CHADEMA na CUF ni vigumu kuogelea ndani ya rangi hizo!!!

    ReplyDelete
  3. JK angalau angemrudisha Mzee Lyatonga ktk Baraza la Mawaziri kwenye Wizara ya Mambo ya ndani Ulinzi Shirikishi!

    Nani asiyefahamu Upolisi anauweza?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...