NA EVELYN MKOKOI

Kuongezeka kwa kina cha bahari, kuongezeka kwa gesi joto, kupungua kwa barafu hususan katika mlima Kilimanjaro na mabadiliko ya mfumo ya mvua, Imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi nchini.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira, Bw Richard Muyungi katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo wa biashara ya hewa ukaa, mjini Bagamoyo iliyohusisha wataalam wa masuala ya mazingira kutoka katika sekta mtambuka nchini.

Bw. Muyungi ameeleza kuwa, Shughuli za kibinadamu hasa katika nchi zilizoendela kama vile za uzalishaji viwandani zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta athari za mabadiliko ya tabia nchi..na hii inatokana na kuachiwa kwa kiasi kikubwa cha hewa ya ukaa kutoka viwandani kwenda angani, ambapo ongezeko la joto ni kichocheo kikubwa cha athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Bw. Muyungi aliongeza kuwa uzalishaji wa gasijoto katika maeneo mengine, kama misitu, kilimo, joto, usafirishaji, majengo na methane huzalishwa kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizoendelea na uleta athari za mabadiliko ya tabia nchi.

”Katika nchi zinazoendelea umaskini ndo unasababisha ukataji ovyo wa misitu na kuiuza kwa bei rahisi, aidha matumizi mabaya ya mbolea katika sekta ya kilimo huchangia pia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gesi joto.”

Alisisitiza Tanzania ni nchi mojawapo iliyoridhia mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi tangu mwaka 1996 na itifaki ya Kyoto ya mwaka 2002 ukiwa na lengo kubwa la kupunguza uzalishaji wa gesijoto.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (kushoto) akifungua warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa mkaa, na athari za mabadiliko ya tabia nchi,mjini Bagamoyo leo.(kulia ni Injinia. Ladslaus Kyaruzi Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais.
Baadhi ya washiriki, wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa mkaa mjini bagamoyo leo.
Picha ya washirki wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa Biashara ya hewa mkaa mjini Bagamoyo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...