MHE.
SOPHIA M. SIMBA (MB)
WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto inaadhimisha miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, ambayo
yatafanyika kuanzia tarehe 27 Januari 2014 mpaka tarehe 31 Januari 2014.
Maadhimisho ya miaka
50 haya yataenda sanjari na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wizara utakaohusisha
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa na
Wilaya kutoka Tanzania nzima wanaofanya kazi katika Halmashauri zetu, Wakuu wa
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Wadau
wengine.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA 2014 NI;
“Taaluma
ya Maendeleo ya Jamii: Nyenzo Muhimu katika Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini
wa Kaya”.
Vilevile kutakuwa na
maonesho ya kazi za mikono, kutoka
katika vikundi vya wanajamii wa Halmashauri za Arusha na Arumeru. Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) watafanya maonyesho, pia watatoa huduma za afya
kwa jamii.
Hivyo, wanakaribishwa
wadau na wananchi wote kwa ujumla kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Tengeru.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA NA WATOTO KWA HISANI YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...