Home
Unlabelled
MAFANIKIO YA WIZARA YA MAMBO YA NJE - MWAKA 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hivi waziri unaposema mnajivunia kupata pesa ya msaada wa milenia kama vile ni kitu cha sifa sana ni sahihi kweli?.hivi kweli na rasilimali zote tulizonazo na uhuru wa miaka mingi bado tunaona sifa kutegemea jasho la walipa kodi wa nchi nyingine??
ReplyDelete..ni hivi hili suala la kufurahia msaada ni baya na la aibu kubwa sana..ni fedheha nzito kama vile tunavyoona aibu kwa kuwa na ombaomba mitaani wakati tunakila kitu kama nchi. Ninaomba hata kama tunapokea basi iwe kimyakimya tusijidhalilishe kwa kuitangaza na kuifurahia hali hii.
mdau UK
Hongera sana Waziri Bernard Membe kwa kazi nzuri na maelezo mazuri ya maendeleo katika wizara yako. Mungu azidi kukupa nguvu kwa kuipenda nchi yetu ya Tanzania na kuwa chachu ya maendeleo. Asante na maendeleo yazidi zaidi
ReplyDeleteMdau UK. Hiyo siyo misaada ni mikopo. Ukisikiliza vizuri utakia tumepewa misaada kwa 'masharti nafuu'. Kwa hiyo siyo misaada ya bure kama mfano wa ombaomba. Mtazamo wangu naona kama ni matumizi ya lugha kusema msaada sounds better than mkopo.
ReplyDeleteSasa naomba maoni, lipi baya zaidi.
1. Serikali kuchukua msaada
2. Serikali kuchukua mkopo
Mdau 1 Misaada ya kiuchumi kufikia malengo ya milenia ni muhimu hata nchi zinazoendelea
ReplyDeletezinasaidiwa mikopo(without conditions)kutoka World Bank fanya utafiti kabla ya kulaumu juhudi za uongozi wa serikali na wizara ya mambo ya nje zimeleta maendeleo ya mafanikio makubwa saana kwa Taifa letu bado changa.
Mikidadi-Denmark
Nakubaliana na madau wa kwanza kabisa,Tanzania imekuwa ombaomba wa kutupwa na Rais na uongozi mzima unatkia aibu unapokuja kuomba huku nje.Kuna nchi ndogo sana hapa Duniani na zina rasilimali ndogo lakini hawaombi kama Tanzania.Hata kama mikopo yenu masharti nafuu ila misaada mingi sana tunapewa na asilimia nyingi ya bajeti ya Serikali inaendeshwa kwa misaada na omba omba.Kuna nchi kama Finland natoa mfano mmoja tu,haina rasilimali nyingi lakini ni wachapa kazi na wemeendelea.Ona Malaysia,kwa Afrika Botswana,Cape verde,Mauritius,seycheless.Je hawa wanashinda resources za Tanzania.Jibu hapana je kwa nini sisi ni omba omba?
ReplyDeleteHichi kikazi kinaona Baba anaomba na watoto wanajifunza kuomba kutoka kwa Baba.Kwa hiyo msitegemee mapya kwa kikazi kingine itakuwa kuomba hadi Yesu akirudi.Taifa sio changa lina miaka 50 ni mingi na lazima tujizikie aibu kuomba.hili suala la mikopo ni asilimia ndogo asilimia kubw ani kuomba.Na kwa nini muwe mnakopa tu ?Wakati hamna uwezo wa kulipa hayo madeni?Si kuuza uhuru wenu?Nchi zingine ziliendelea hapa duniani kama zingekubali kuwa omba omba kamwe sizinge endelea.Kuna mtu mimi aliniuliza kwa nini nyie ni masikini wakati mna malighafi nyingi.Nakuahidi kama kungekuwa kuna uwezo wa kubalishana nchi na watu wake ,tungewapa watu wa nchi ingine ambao wako makini ,na sisi tukahamia nchi yao ambayo imeendelea.Matokea nchi iliyoendelea WaTanzania wangeirudisha kuwa nchi masikini na nchi yetu ingeendelea.
Ona Makaburu walivyoendeleza Afrika ya Kusini na Namibia.Australia ilivyoendelezwa na Waaustralia weupe na New-zealand alivyoendelezwa na wahamiaji weupe.WaTanzania kama taifa hatuko masikini na ndio maana bado ni omba omba,kwa sababu hatuwezi kufikiri.
Mtoto wa Kabwela,Sweden