Salaam aleikum kwenu Wadau wetu wapendwa.
Timu
nzima ya Michuzi Media Group Ltd (MMG)ambao ni wamiliki wamitandao pendwa ya
kijamii ikiongozwa na Libeneke la Globu ya Jamii Michuzi Blog,Jiachie
Blog na Mtaa kwa Mtaa Blog pamoja na ile ya Michuzi Matukio, inawatakia
Heri ya Mwaka Mpya wa 2014 Wadau wote popote pale mlipo,kwa kuwa pamoja
na timu hii kwa kipindi chote tangu timu hii ilipoanza kuingia mitamboni
miaka kadhaa iliyopita.
Kwakweli tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi kwa kuweza kutufanikisha kuuona Mwaka huu Mpya wa 2014 tukiwa hai na wazima wa afya,kwani kuna wenzetu wengine hawajaaliwa kufika siku hii,hivyo kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu,tunapaswa kumshukuru sana.
Kwakweli tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi kwa kuweza kutufanikisha kuuona Mwaka huu Mpya wa 2014 tukiwa hai na wazima wa afya,kwani kuna wenzetu wengine hawajaaliwa kufika siku hii,hivyo kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu,tunapaswa kumshukuru sana.
Timu
nzima ya Michuzi Media Group Ltd (MMG)inawatakieni kila la kheri katika
Mwaka huu mpya wa 2014 na Mwenyezi Mungu atujaalie sote uwe ni mwaka wa
mahanikio kwa kila mmoja wetu.
Ahsanteni sana
Tuko pamoja Ankal.....hii platform - MMG Ltd wakati wote imetuleta pamoja sana kwavile wakati wote tuko "live" tumeunganishwa kinamna yake sana hapa kwani wada wote yaani wale wa diaspora (the mduduz + wakuu wangu wengine huko duniani) na wale wana-libeneke wa kule kanyigo, nyarugusu, mbamba-bay, tandahimba n.k. tunaweza kushiriki mijadala kana kwamba tuko "round table"; msaada kwenye tuta; hoja ya haja....hili ni jambo la kujivunia sana na lazima tumshukuru MUNGU kwelikweli.... kila la heri kwako & timu yote ya MMG Ltd .... MUNGU atujaalie sote afya njema na imani katika kumcha MUNGU, 2014 uwe mwaka wa heri, baraka & mafanikio kwetu sote.
ReplyDeleteSwadakta! Tunashukuru!
ReplyDeleteNami nakutakia safari njema ya siku hizi nyingine zipatazo 365 na robo na hata zaidi!
NB:
Tunaomba uwe unaziposti komenti zetu hata kama zitamuuzi mtu FULANI ilimradi hatutoi lugha ya matusi!
Kauli Mbiu:
Tunapoelekea uchaguzi mkuu ujao, tunaomba wanasiasa ambao wanalazimisha tuwakubali hata kama hawana vigezo wajitoe wenyewe. Tusitumie vibaya nafasi tuliyopewa(na hasa pengine kutokana na migongo ya wazazi wetu) kujifanya sisi tunajua sana au tunajua kufanya mazoezi ya siasa kwa kuiga mafanikio ya wanasiasa fulani wa nchi fulani(e.g OBAMA Wannabe)!
STOP YOUR SUPERIORITY ATTITUDE/COMPLEX, CHEAP, CHILDISH AND MANIPULATIVE POLITICS!!
TANZANIA HAS MORE THAN 40 MILLION PEOPLE, many ARE CAPABLE more than you BUT SIMPLY THEY DO NOT HAVE THAT "god FATHERS" TO LET THEM UP
GROW!!! (YOUR APPROACH IS SO OFFENSIVE, MAY BE YOUR WIFE DOES NOT TELL YOU)
Alaykum Salaam MMG!
ReplyDeleteSawa Salamu za Mwaka Mpya 2014 tumezipokea, je ni vipi kuhusu Mnuso?
Hata Maandazi na Chai atupati Wadau?
Si mchezo kuumaliza mwaka (NYUNDO MOJA) salama!!!
Mngetuandalia angalau Chai na maandazi pale Sports Lounge City Centre kwa sisi tuliopo Darisalama !!!
Ankali namuunga mkono Mdau wa 3 juu ya Takrima na swadaqa ya chai na maandazi!
ReplyDeleteAlaykum Salaam!
ReplyDeleteMjomba Michuzi siku zote Uungwana ni vitendo!
Na sio maneno na salaamu za mwaka mpya kavu kavu!
Ni kiasi cha kuandaa kwa kuituma Kampuni ya Catering kuandaa makapu mawili au matatu ya maandazi na themosi moja au mbili za chai ''sio vinywaji ghali sana kama yale maji makali yanayouzwa kwa fedha nyingi''.
Sehemu ya shughuli kukwepa gharama unaweza kuwaomba NBC-Bank watupatie ile Bustani yao pale Posta Baharini patatosha sana!!!
Heri ya mwaka mpya 2014 na ninyi MMG!!
The mdudu Kaka kuona,,mdau hapo juu huo ndio uzalendo uliotukuka unajua kutoa maoni kuhusu nchi yetu na watu wake ni kitu muhimu sn kwa mfano mm haipiti siku bila ya kuingia M.M.G na kutoa yalio moyoni juu ya nchi yangu na ndugu zangu watanzania,mm kivuri ndio kipo ugaibuni lakini mwili wangu wote uko huko nyumbani,,angalizo kwa wadau au hata mjomba Michuzi nakuombeni mnitumie FULANA YA MICHUZI BLOG ili nijivinjali nayo huku ugaibuni coz ndugu zangu wananiangusha sn na hilo swala,,asante sn MMG kwa kutu wish na New year nanyie pia heri ya Mwaka mpya,na watanzania wote popote walipo nawatakia heri ya 2014
ReplyDelete