Binti Aida Nakawala (miaka 25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya,akiwa na watoto wake wanne aliojifungua hivi karibuni katika hospitali ya Wazazi ya Meta,Jijini Mbeya.Mama huyo alijifungua Watoto hao wa wanne kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya na anaendelea vizuri kabisa.Mama huyo jana alitembelewa na baadhi ya Wadau wa Habari wakiongozwa na Mwanalineneke wa Blog ya Mbeya Yetu,Joseph Mwaisango,ambapo waliwasilisha mchango wao mdogo waliokuwa nao,wengine alioambatana nao katika kuwasilisha msaada huo ambao ni pesa taslim,simu ya mkononi na nguo za watoto hao toka kwa wasamaria wema ambao ni Yassin Kapuya , Hassan Othman,Mwanalibeneke Othman Michuzi pamoja na Dada Pendo Fundisha.
Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog (kulia) na Dada Pendo Fundisha wa New Habari (kushoto) wakiwasilisha msaada wa nguo kwa Mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja,Bi. Aida Nakawala.
Mdau Ezekiel Kamanga pamoja na Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog wakikabidhi msaada wa pesa taslim pamoja na simu ya mkononi kwa kwa Aida Nakawala,mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja.Utaratibu wa kumpatia mama huyo namba ya simu unafanyika hivi sasa na iwapo itakuwa tayari italetwa hapa hapa ili kwa yeyote atakaetaka kumsaidia mama huyo,aweze kufanya hivyo.
Wakipata maelezo ya Maendeleo ya Mama huyo kutoka wa Muuguzi,Terecia Bahari (kushoto).

Baadhi ya wadau waliomtembelea mama huyo hospitali ya Wazazi ya Meta,jijini Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. nilikuwa nawawaza hao watoto mungu awabariki sana,mliotoa mzidishiwe mara dufu

    ReplyDelete
  2. Thanks Mbeya yetu, good example.
    The MPESA number please Mr Michuzi? Make this as effective and efficient fundraising to start 2014? Giving to those who really need.
    Asanteni

    ReplyDelete
  3. Mungu awabariki sana wote mlioguswa na hili na mnaoendelea kumsaidia mama huyu. Kwa kweli watanzania tupo waungwana sana. Mungu azidi kuwabariki sana

    ReplyDelete
  4. Nafikiri m-pesa,,tigo pesa au airtel money akaunti zingetolewa kwenye blog, zingesaidia sana. Kwa watu ambao wako mbali na wangependa kuchangia.

    ReplyDelete
  5. The mdudu,naisubili kwa hamu hiyo number,,mjomba Michuzi plz livalie njuga hili swala wapigie hodi wafanyabiashara wakubwa wote,kuanzia MENGI wa IPP,Baharesa wa AZAM TEAM,Y,MANJI,MO wa METL,na wabunge wote na wakuu wa mikoa,Mawaziri achilia mbali hivi vijisenti vyetu ijapokua vitamsaidia kwakiasi flani,,lakini hilo kundi nililokwambia hakiamungu MAMILIONI YA PESA YATAPATIKANA trust me mjomba,kumbuka Mjomba MICHUZI ww ni mtu Maarufu sn hapo Tanzania kwahiyo tunakuomba kitu chochote kinachohusiana na mambo ya nchi yetu na watu wake na maendeleo yake basi ww ndio uwe mwakilishi wetu wa kwanza coz ww ni KIO CHA JAMII,

    ReplyDelete
  6. Mungu awabriki kama alivyosema mdau tupe m-pesa tuchangie, ila naomba ni sahihishe, kwa kizungu ni quadruplets sio quadliplets

    ReplyDelete
  7. Where is the father of the kids?

    ReplyDelete
  8. Pale unapofikiria ubinadamu umekwisha... Endeleeni kazi nzuri hii familia inahitaji msaada wowote uliopo. Ndugu unaeuliza baba wa watoto, think twice... ungekuwa wewe labda ungemkimbia huyo mama. Watoto wanne kwa mkupuo sio lelemama... na ndio maana michuzi na wengine woote wanaomuombea huyu mama msaada wamefanya hivyo. Kwani hujaona humu watu wakiwapigia harambee watu waliojaliwa mtoto mmoja au wawili...!!! So that tells you how important this whole issue is haswa huku bongo kwetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...