Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea eneo la Dumila ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu sehemu ya barabara kwenye daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro.

Akiwa katika eneo hilo Waziri Magufuli baada ya kujionea hali halisi amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Crispianus Ako pamoja na Watendaji wengine waandamizi kutoka Tanroads na Wizara ya Ujenzi kuwepo hapo muda wote wakati kazi za kurejesha mawasiliano zikiendelea ili kuhakikisha kuwa matengenezo hayo yanakamilika kesho siku ya Ijumaa tayari kwa magari kuanza kupita.

Katika hatua nyingine Mhe. Magufuli ametahadharisha kuwa magari yanayoruhusiwa kuzungukia barabara mbadala inayoanzia Dumila kupita Kilosa hadi Morogoro ni mabasi ya abiria na magari mengine yasiyozidi uzito wa tani 10. “Barabara hii mbadala ya kupitia Kilosa, Melela hadi Morogoro ni ya mkoa na iko katika kiwango cha changarawe ikiwa na madaraja yenye uwezo wa kubeba chini ya tani 10 tu, hivyo magari mengine yote yenye uzito zaidi ya hapo yatabidi kusubiri wakati tukiendelea na jitihada za kuifungua barabara hii mapema iwezekanavyo” amefafanua Mhe. Magufuli.

Daraja la Mkundi liko kiasi cha kilometa 65 kutokea Morogoro mjini kuelekea Dodoma na mikoa mingine ya kati hadi magharibi mwa nchi yetu ikiungana na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya watu wa Kongo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa watendaji wa Tanroads.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anafuatilia kazi katika moja ya mitambo ya barabara.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ukaguzi wa eneo lililobomolowa na mafuriko ya mvua katika daraja la Mkundi, Dumila mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa madereva wa Lori zinazofanya kazi katika eneo hilo.
Mtambo ukiwa kazini
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza dereva wa lori kumwaga mawe sehemu husika.
Muonekano wa Daraja hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu,,yeeees piga kazi RAIS wetu 2015 nashangaa wanaojitesa na MICHOPA huku wakijua rais ni huyu mm sio kama sipendi mabadiliko au vyama vya upinzani lahashaaa tatizo lao kubwa wao hawashiliki kwenye mambo ya kimaendeleo kama hayo wao wanajua upinzani ni kuponda kila kitu kumbe wala,,unajua nini? Baba atakua baba tu hatakama humpendi ndio maana muda wa kula husahau yote na taratibu unajisogeza kwenye kuyakata matonge

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...