Kutokana na ugunduzi wa gesi asilia na mafuta nchini, Tanzania imeonekana kuwa na thamani kwa nchi mbalimbali duniani na kuiangalia nchi hii kwa namna tofauti na ilivyokuwa awali kwani sasa imeonekana kuwa na utajiri mkubwa.
Ugunduzi huu umepelekea Wizara ya Nishati na Madini kupokea wageni wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika ili kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara baina ya nchi husika.
Hivi karibuni wizara ya Nishati na Madini imetembelewa na ujumbe toka Jamuri ya Czech nchi ndogo miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika kwa lengo la kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Ujumbe huu uliongonzwa na Bw. Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya Nchi ya Czech aliyeelezea uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na madini na kusema kwamba awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa maji, gesi pamoja na nishati jadidifu, na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.
Dub alieleza kuwa maendeleo si tu kutegemea utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia bali inatakiwa nchi ifanye nguvu ya ziada katika kuongeza thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu kwa kujenga viwanda jambo lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.
Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka Wizara kuelimisha watanzania katika chuo cha madini katika nchi hiyo na kwamba mawasiliano yataendelea kufanyika ili kufikia malengo ya uhusiano huo.
Kwa upande wake Masele amesema kwamba zipo fursa nyingi za uwekezaji nchini katika sekta ya madini na zaidi madini ya viwandani lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia ugunduzi wa gesi na mafuta vitalu vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech kuomba vitalu hivyo ili kuweza kushiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...