Mbunge wa Viti maalum Jimbo la Iringa akizungumza na wananchi hawapo pichani kuelezea kazi alizofanya katika jimbo la Iringa katika mkutano uliofanyika katika kiwanja cha Mwembetogwa.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa ccm katika kiwanja cha mwembetogwa
Baadhi ya wanachama vijana wa chadema waliorudisha kadi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ccm wilaya katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)
=========  ========  ===========
MBUNGE LITA KABATI AELEZA ALIYOYAFANYA HADI SASA KATIKA UBUNGE

Na Denis Mlowe,Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rita Kabati ameeleza kazi mbali mbali alizozifanya katika jimbo la Iringa mjini ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi kilichoko jirani na chuo Kikuu cha Iringa(Tumaini).

Kabati alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kuwa ataendelea kutatua  kero za wananchi wa Iringa mjini kila anapopata nafasi za kuwahudumia wananchi hao.

Alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa siku zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa siku zote kwake atahakikisha anatenda zaidi na amekuwa akijenga hoja za kusaidia Jimbo la Iringa mjini na sio kutoa kejeli kwa serikali akiwa mbungeni .
Akielezea mambo ambayo amepata kutekeleza alisema ni pamoja na kusaidia sekta ya elimu vitabu na kompyuta pamoja na kusaidia vikundi vya vikoba katika jimbo hilo la Iringa mjini kusaidia vijana katika harakati za kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha mashindano ya Kabati Star Search.

Kwa upande wake katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga alisema yeye alikuwa jimbo la Freeman Mbowe ambae sasa anatangaza kutogombea jimbo la Hai.

Alisema zama za ubunge wa Mchungaji Peter Msigwa katika jimbo la Iringa mjini umekwisha na sasa atake ataondoka na asipotaka ataondoka.

"Mwambieni mbunge Msigwa wakati  wa kuwadanganya wananchi umekwisha  na lazima sasa awaeleze wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  wapi  anapelekea fedha za mfuko wa  jimbo ambazo  zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya  Kikwete"

Hata  hivyo alimuagiza meya  kupambana ili  fedha  kiasi cha Tsh milioni 15  zinazotolewa na rais Kikwete kuona zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge  pia kutembelea  Hospital  na vituo vya afya  ili  kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu kupeleka majibu katika ofisi yake.

Aidha aliwataja  vijana  kuleta maendeleo  ya mji wa Iringa na sio vijana  wa kutumiwa kuvuruga maendeleo ya mji wa Iringa.

" Nawaombeni  wananchi  kuwa tayari  tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba  wananchi tusaidiane kumnywesha panado na ninamuomba  Msigwa fedha za kiinua mgogo  zake asije  tena katika jimbo la Iringa mjini atumie  kwa kazi nyingine  ....tumeanza mkakati  huu kwa ajili ya kumng’oa Msigwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani tunajua kama Kiswahili chetu kina mgogoro katika baadhi ya matamshi lakini kwa majina ya watu tuwe makini sana.Huyu mama anaitwa Rita Kabati sio Lita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...