Kwa Jina naitwa Osman Bairu ni Mwanamichezo na Mwalimu wa Mchezowa Kriketi (Cricket),Nilianza kucheza mchezo huu wa Kriketi nikiwa na umri wa miaka sita(6) nilipokuwa nchini India katika shule ya msingi iitwayo Barnes school.
Nilipokuwa shuleni India nilivutiwa na timu ya Taifa ya WEST INDIES na mchezaji aitwae VIVIAN RICHARDS ambaeni Keptein wa timu ya taifa ya WEST INDIES.
Katika kipindi cha Mwaka 1984 Nilifanikiwa kucheza katika timu ya shule katika nchi ya Panchigan
-1996 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka kumi na saba(17) mjini Mombasa,nchini Kenya na baadae mwaka 1998 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania-Uganda nikiwa Mwafrika peke yangu.
Mwaka 1996 nilipata kushinda na kuwa mchezaji bora wa kuchipukia kutoka katika chama cha Kriketi (Cricket) Tanzania nikiwa Mwafrika wa kwanza.
-Nina cheti cha ushiriki katika Kriketi kutoka Alayans Kriketi ligi ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...