Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bwana Clement Mshana (kushoto) akimpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia wakati wa mapokezi yake katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam leo katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Elisante Olegabriel.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bwana Kulwa Magingila wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fennela Mukangara akimkaribisha Naibu Waziri Mheshimiwa Juma Nkamia katika Ofisi za Wizara zilizopo katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na Wanahabari Ofisini kwake katika tukio la kumkaribisha lililofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Prof Elisante Olegabriel.Picha na Benjamin Sawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Inapendeza, sasa fanyeni kazi!

    ReplyDelete
  2. Mimi naona wizara hii serikali ijayo iangalie upya, vijana, habari, utamaduni na michezo, hivi vitu vinne haviendi pamoja. Ukiangalia tatizo la vijana kwa sasa ni kazi na utamaduni, sababu kutokana na utandawazi wanaiga haraka sana tamaduni nyingine, kwa hiyo wanahitaji malezi na maelekezo kujua utamaduni wao na kuulinda. kwa hiyo wapelekwe kule wizara ya kazi, na swala hilo la utamaduni pia. Japo naona hilo la utamaduni lingeunganishwa na wizara inayo husu mambo ya jamii. Kwa ujumla hizo wizara kwa awamu hii hazikupangwa vizuri, na hapo huwezi kupata ufanisi, sababu watu wanaangaliana, labda hili ni jukumu la yule na si mimi.

    ReplyDelete
  3. Mdau No. 2 hapo juu uko sahihi sana .... unajua changamoto tulizo nazo ni kwamba kila prezida anapoingia madarakani anakuja na muundo wake wa cabinet (& wizara) na hivyo hakuna "consistency" ya ki-muundo na hata "content" ya nini kiwepo ndani ya hizo wizara.

    Na unajua kuwa muundo wa hizo wizara mara nyingi unaathari za moja kwa moja juu ya kuongeza matumizi ya serikali...hapo tunazungumzia ukubwa/udogo wa serikali.

    Hata hivyo ikiwa hakuna nia ya dhati ya kujenga utamaduni wa nidhamu ya matumizi bado unaweza ukawa na wizara chache na serikali ikawa na matumizi makubwa vilevile...

    Way Forward: Mjadala wa kina unahitajika kubaini muundo sahahi utakao - "optimize cost" na kuiwezesha serikali kushughulika na mambo ya msingi kwa ustawi na maendeleo ya taifa & watu wake.

    Ingawa hivyo mahitaji & vipau mbele vinavyolingana na wakati unaohusika si jambo la kulipuuza pia.

    ReplyDelete
  4. Hawa wanahabari nao wanafiki juzi alipotangazwa jina lake wakaguna na kuanza kucheke eti "hata huyo" leo naona wameunga tela ofisini kwa mzee na kutoa shikamoo nyingi kama ManU walivyokuwa wanamwamkia sir Etoo..lol

    ReplyDelete
  5. Kila nimuonapo prof.Elisante Ole Gabriel nakumbuka darasa lake la mwisho wakati anteuliwa na Raisi pale mzumbe university. Alisema "there are three kinds of people with regard to minds; Great minded people,average minded and simple minded" Aliwaelezea zaidi kwa kusema "Great minded people want things happen and they participate in those change, Average minded want to see changes but they don,t want to be party,and simple minded people always have no direction and wonder why things are happening"
    Prof Gab endelea na kazi na hakika wewe ni jembe.

    ReplyDelete
  6. Naona chenga tu!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...