Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akimtambulisha dada zake,wakati Mh Lowassa alipokwenda kumpa pole Mzee Makamba aliepatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Mh. January Makamba wakati wa mazungumzo yao.Mh Lowassa aliitembelea Familia ya Mzee Makamba kwa kumpa pole kwa kupatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
duuuh white hair katupia kitu cha jeans pale katiii!!
ReplyDeleteMnaweza watu wawili totauti kila mmoja akiwa kitandani kwake sehemu mbili tofauti lakini cha ajabu mnaweza kuota NDOTO INAYOFANANA!
ReplyDeleteMhe.Edward Lowassa anayo ndoto ameota juu ya kuwapatia Watanzania neema na pia Mhe. January Makamba anayo ndoto pia kuwawezesha vijana na Watanzania kwa maisha bora!
Hahahahahahah Mdau wa Pili umenichekesha sana!
ReplyDeleteLa ajabu jingine mnaweza kuota ndoto watu wawili mwingine ndoto zake zikatimia na mwingine zisiwe kabisaaa.
Na mwingine anaweza kuota ndoto badala ya kuwa ndoto akajikuta anazama ktk Jinamizi!