Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbande(mwenye suti nyeusi) akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi katika benki hiyo Tumsifu Invocarith ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbande(mwenye suti nyeusi) akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi katika benki hiyo happness msengi ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao walivyokabidhiwa kama sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi mbalimbali walizokabidhiwa baada ya kufanikisha tawi hilo kuwa miongoni mwa matawi yaliyopata mafanikio katika kipindi cha muda mfupi.
Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakigonga Cheers kufurahia mafanikio katika tawi hilo.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

MENEJA wa benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmbande amepongeza uongozi wa benki hiyo ambao pia ni wakurugenzi kwa kuwezesha tawi hilo kuwa miongoni mwa matawi yaliyopata mafanikio ndani ya kipindi kifupi.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 iliyoenda sanjari na pongezi kwa wafanyakazi wa tawi hilo Bi Mmbande aliwapongeza wakurugenzi hao ambao ni mifuko ya hifadhi ya jamii, NSSF,PPF,PSPF,LAPF na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki(EADB) pamoja na wanahisa wengine.

Aliipongeza pia Kurugenzi ya Azania bank chini ya uongozi wa Bw Charles Singili ,watumishi wote wa banki ya Azania hususani wale wa tawi la Moshi pamoja na wateja wote wa banki ya Azania kwa ushirikiano wao wa pamoja ulioowezesha kupatikana kwa mafanikio hayo ndani ya kipindi kifupi toka kufunguliwa kwa tawi hilo mjini Moshi .

Bi Mmbande alitoa rai kwa kila mdau wa benki ya Azania kuongeza ari ,kasi na ushirikiano katika mwaka huu mpya wa 2014 ili kuifanya benki ya Azania iwe bora zaidi na kufikisha huduma kwa kila mtanzania kama ambavyo inavyojitangaza kwa watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...