Kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu 2014, lile tamasha kubwa la Nyama choma linalofahamika kama The Nyama Choma Festival (TNCF) limepangwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014. 

Nani alifikiria kuwa Nyamachoma ingeweza kuwaleta maelfu ya watu pamoja? Toka lilipoanzishwa,  tamasha la nyama choma ambalo limesajiriwa kisheria limekuwa ni sehemu ya kipekee ya kuweza kufurahia aina mbalimbali za nyama choma na pia ni eneo linalowakuwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali wanaofika kufaidi nyama zinazochomwa na wataalamu wa kuchoma nyama kutoka katika kona mbalimbali za jiji la Dar salaam kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu.

Ukiachana na aina mbalimbali ya nyama zinazokuwepo katika tamasha hili, hii pia ni sehemu mojawapo ya kufurahi na marafiki ikiwa ni pamoja na “mtoko” kwa familia kwani huduma zinazotolewa zimezingatia umri wa watu wote yaani kuanzia watoto hadi watu wazima. Kuna eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya michezo ya watoto, vinywaji vya ain azote na burudani nzuri ya muziki. Si hivyo tu wapo watu wengine wanaotoa huduma za kahawa, ice cream, michoro ya usoni, vyakula vya kawaida na michezo ya nje ya watuwazima kama pool n.k

Tupo katika dunia ambayo inatulazimu kuwa katika mtandao mkubwa na watu wenye weledi tofauti, The Nyama Choma Festival inakuwezesha kuingia katika mtandao huu kwa urahisi zaidi. Kwani kwa siku hii moja tu watu wote wanaweka vyeo na nafasi zao kitaaluma pembeni na kuchanganyika na watu wote huku wakifurahi kwa pamoja. Katika hali hii watu wanabadilishana uzoefu na kupeana mawasiliano kwa ajili ya siku za usoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...