Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji, kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni 25.4.Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kikao hicho.Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...