(kushoto)
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa) kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.
Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.
Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri.
Alisema Shiwata itakusanya zaidi ya sh. Mil.7 kutoka kwa wanachama 7,000 na wasanii watajiunga kwa sh. 20,000 ambazo zinaweza kulipwa kwa awamu tatu kutokana na uwezo wa msanii.Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri.
Sjiwata ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari 500 za kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...