Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kukagua maonyesho ya vijana wajasiriamali ya mkoa wa morogoro akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface. Maonyesho hayo ambayo yapo katika mpango wa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana ujulikanao kama Tanzania Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP)  ambao upo chini ya kampuni ya AJ IT Development Company Ltd.
 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka mkoa wa morogoro. baadhi ya vijana hao kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Chuo kikuu Mzumbe, Chuo kikuu cha kiislaam Morogoro. Lengo la maonyesho hayo ni kuzitangaza na kuzitafutia masoko kazi za vijana wajasiriamali. 
 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akizindua tovuti ijulikanayo kama MATUKIO NA VIJANA itakayokua ikiripoti masuala ya kijamii hususani masuala ya vijana, akisaidiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Mipango wa kampuni ya AJ IT Development Company Ndugu Fasali Mwenzegule. Pamoja na uzinduzi huo Mkuu wa wilaya alizindua mitandao mbalimbali ya kijamii itakayotumika katika mpango huu ikiwemo akaunti katika Instagram (@youth_entrepreneurship), twitter (@youth_entrepreneurs) na facebook (Tanzania-YOUTH-Enterprenuership).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...