Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kilimo uliofanyika mjini Davos,Uswisi usiku wa kuamkia leo Januari 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza,Mhe. Niuck Clegg wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Sheraton mjini Davos, Uswisi leo Janaury 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton mjini Davos,  Uswisi leo January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton mjini Davos, Uswisi leo January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah mara baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji salama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa mara baada ya kuhutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji nsalama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Afrika ya Mashariki ina Maraisi Watano (5) ambao ni Yoweri K. Museveni, Paul Kagame, Uhuru Kenyatta, Pierre Nkurunzinza na Ndugu yetu Jakaya M. Kikwete.

    Je, kwenye vikao hivi vya Davos-Uswisi Maraisi wengine wa hii EAC mbona hatujawahi kusikia wakipewa nafasi ya kuhutubia hapo kama JK?, ama haionekani kama kweli huwa wanaalikwa kuhudhuria Vikao hivi?

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Mh. Rais wetu ni regular attendee katika kongomano hii lakini mwaka huu WEF walialika marais 2 kutoka EAC: Mh. JK na Paul Kagame. JK was one of the speakers katika: http://www.weforum.org/sessions/summary/breaking-silos-development lakini hakuweza kuhudhuria kwa sababu ya msiba wa Mbunge wa Chalinze (May Allah rest bless his soul) na Kagame atahutubia leo saa 2.30 EAT: http://www.weforum.org/sessions/summary/next-steps-emerging-economies

    ReplyDelete
  3. Hao Maraisi wengine Afrtika ya Mashariki hawana jipya la kuiueleza Dunia kwa sasa !

    Ni vile wana Misala tofauti tofauti na kuwa wameshakuwa Fungu la Kukosa, yaani hadi Raisi yeyote atakaye shirikiana na akina K-3 lazima atapata Majanga mfano Raisi Salva Kiir wa Sudani ya Kusini hivi sasa mambo yake yameharibika na ana vita kwake.

    Siri ni kuwa akina K-3 wana ushauri mbaya kwa yeyote atakaye shirikiana nao kwa kuwa hawana Rule of Law na Social Justice kimatendo.,,,hivyo mara zote tegemea ushauri mbaya kutoka kwao, pia kutokana na hilo ni lazima mambo yako kama Raisi wa nchi yataharibika.

    Angalieni jinsi Raisi Salva Kiir wa Sudani Kusini alivyo mfukuza Kazi Makamu wa Raisi Dr.Riek Machar ni kuwa hakufuata Kanuni za Uongozi Bora sambamba na Mkataba wa Makubaliano ya awali juu ya Muundo wao wa Serikali miongoni mwa Makundi ya Kikabila Dinka na Nuer.

    Hivyo K-FAIL ni akina K-3 ambao ni Maraisi wa CoW 'Coalition of Wiulling' wakati K-SUCCESS ni akina Kikwete(Tanzania), Nkurunzinza(Burundi) na Kabila(Congo-DRC)!

    ReplyDelete
  4. Ndugu Ali Mdau wa pili hapo juu, elewa dunia ina shawishika na Kiongozi mwenye mafanikio Kiuchumi na pia Utawala bora !

    Huwezi kuidanganya dunia kujenga mafanikio ya kiuchumi wakati unaendesha nchi kwa KIGANJA CHA CHUMA !

    Ni hati hati ktk hii Afrika ya Mashariki yetu ukimwacha JK pana Maraisi wanaweza kumaliza vibaya kulinga na jinsi dunia inavyo watazama na jinsi barometer ilivyo wabadilikia kwa miaka hii michache.

    Ndio maana ktk Genge alilotaja Mdau wa 3 juu hao jamaa K3 tusije kushangaa kuitwa ICC-The Hague !!!, kama mmoja wao anavyo buruzwa huko hivi sasa.

    Angalia tukio la Afrika ya Kusini kifo cha Patrick Karegeya aliyekuwa ktk Utawala wa Kigali miaka iliyopita!,,tazama Barometer inavyo badilika sasa kutokana na kifo hicho...HATUTOI UCHURO LAKINI PANA DALILI MBAYA.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa pili POUL KGM amesha anguka ananuka damu!

    Alivyo sasa mbele ya Jumuiya ya Kimataifa siyo kama alivyo kuwa mwaka juzi 2012 kabla hajakataa Ushauri wa JK!!!

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana kabisa wadau wenzangu. Lazima tuwe na utawala bora uliotukuka.

    This may be of interest to some:

    "For several hours on Friday morning [January 2014], a false rumour that the Rwandan President Paul Kagame had died spread like wildfire in the city of Goma, in the east of the Democratic Republic of Congo - prompting scenes of celebration. It appears to have been triggered by a fake post on Facebook". http://www.bbc.co.uk/news/blogs-trending-25682683

    Video: https://www.youtube.com/watch?v=L9EPcUOpT1M#t=28

    Katika kitabu cha "An Ordinary Man" kilichoandikwa na Paul Rusesabagina - ambaye alikuwa "A moderate Hutu" na aliokoa maisha ya waTutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 94 ameandika:

    "Rwanda is today a nation governed by and for the benefit of a small group of elite Tutsis... Those few Hutus who have been elevated to high-ranking posts are usually empty suits without any real authority of their own. They are known locally as Hutus de service or HUTUS FOR HIRE."

    Kusoma kitabu: http://books.google.co.uk/books?id=yfDv-I_kb7UC&pg=PA254

    Sisi kama waTZ tuna laani kundi la Interahamwe ambao walikuwa na itikadi za kulia (far right). Kwa hiyo sio waHutu wote walishiriki katika mauaji.
    Si kweli kabisa kwamba waliokufa ni waTutsi tu bali hata waHutu waliokuwa "moderate" walikufa, ingawa wengi walikuwa waTutsi.

    Ni imani yangu kwamba Rwanda ikiwa na uchaguzi ulio wa huru na wa haki, mi sita-hesitate kusema kwamba kundi la watu wanao ongoza kwa ukabila watashinda! Hii ni undeniable fact! Mwishoni, mi nadhani bara la Afrika kwa nchi ambazo ni "matata" lazima katiba iruhusu "quota" systems zitakazo rushusu mfumo wa serikali za umoja. Mifano iko mbele yenu: Sudan Kusini. Hii system ya wazungu ya 50% +1 vote si lazima ita-work vizuri kila mara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...