Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na  Januari 18, 2014 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa.
Wakulima na wananchi kutoka Bahi ambako Mheshimiwa Betty Mkwasa anafanyia kazi walileta kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti lita zaidi ya 30, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, bata Mzinga na nafaka za mahindi na mchele kwa maharusi.  
   Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dodoma wakiwa na wake zao wakipiga picha na maharusi. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Bahi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana, Mr & Mrs Sixmund tunawatakia maisha marefu zaidi katika ndoa yenu.

    Mlipendeza sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...