Marehemu Mohamed Chimsala (Danny) enzi za uhai wake
Familia ya Kanali Chimsala wa Jeshi la wananchi Tanzania anaeishi Masaki Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Mohamed Chimsala (Danny) ambaye alikuwa ni askari Polisi kitengo cha Trafiki Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kilichotokea leo asubuhi katika hospitali ya Jeshi la polisi Kurasini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa kaka yake huko Masaki Dar es salaam.
Taarifa zaidi za taratibu za mazishi mtazipata baadae, baada ya familia kukaa kikao.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba:-
"in lillahi wa inna ilaihi rajioon"
"Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe"
Amen.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...