JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME ametoa tahadhari kwa
wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuwa na tahadhari katika kipindi hiki cha mvua
zinazoendelea kunyesha maeneno mbalimbali.
Ametoa
thahadhari hiyo baada ya kutokea tukio la PHILIPO
SUNGURA, Miaka 55, Mgogo Mkazi wa Kijiji cha Mpinga Kata ya Kigwe Wilayani Bahi kufa maji wakati akijaribu kuvuka
mto Mpinga ambao ni wa msimu. Tukio hilo lilitokea tarehe 24.01.2014 majira ya
saa 18:45 jioni wakati akijaribu kuvuka mto huo huku maji yakiwa ni mengi.
Kamanda
Misime ameeleza imembidi kutoa tahadhari hiyo kwani kumbukumbu zinaonyesha watu
wengi hupoteza maisha inapofika msimu wa mvua wakiwemo watoto wanaokwenda kuoga
na kuchota maji katika mabwawa, mito ya msimu na madimbwi yaliyotuama maji kwa
kunasa kwenye tope na kupoteza maisha.
Mfano
anaeleza tangu mvua za msimu zilipoanza mwaka huu 2014 watu wanne (4) wameshapoteza maisha.
Amewaomba
Viongozi wa Mitaa, Vitongoji, Vijiji, Kata, Tarafa na waalimu mashuleni
kuwaeleimisha wananchi na wanafunzi ili kuepukana na matukio hayo.
[DAVID A. MISIME - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
nice info...
ReplyDeleteKtk miaka yote ni leo tu ndio nimefarijika kuona Tangazo lililojaa Uzalendo na Uwajibikaji...
ReplyDelete