Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira ya Bunge la New York, Bw. Robert K. Sweeney akiongoza mkutano ( public hearing) aliouandaa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufanisi wa sheria na kanuni zinazodhiti biashara ya pembe za tembo katika New York, mkutano huo ulifanyika siku ya Alhamis. New York ndiyo inayoongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha Biashara ya pembe za tembo na biadhaa zake katika mwaka 2012 pembe za tembo zenye thamani ya dola milioni mbili zilikamatwa.
Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine alielezea jitihada zinazofanywa na serikali katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo.
Bw. William C. Woody ( mwenye tai ya njano) Naibu Mkurugenzi kutoka Ofisi inayosimamia sheria akiwa na Bw. Richard G. Ruggiero Mkuu wa Kitengo cha Afrika, Uhusiano wa Kimataifa , huduma za Samaki na Wanyamapori nchini Marekani. Wakitoa ushuhuda wao kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika udhibiti na usimamizi wa sheria zinahusu biashara ya pembe za tembo na wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka.
Angalia vikao vya UN watu wana maguduria ya maji. Sisi mikutano yetu machupa kibao ya maji. Hizi chupa zinachangia uchafuzi wa mazingira.
ReplyDelete