Habari za mchana ndugu wanahabari, 
Tumewaita ili kutoa taarifa kwa wananchi juu ya tukio ambalo limetokea ndani ya Mkoa wetu ambalo kwa kiasi kikubwa linataka ufafanuzi kutokana na jinsi linavyozungumzwa huko nje. 
 Siku ya tarehe 13/01/2014 majira saa 9:55 jioni hapo Rahaleo kwa Mchina Tambi palitokea tukio la unyangani wa kutumia silaha. 
Tukio hili lilitokea wakati Bw: SAID SEIF SALAMI 34, Riami wa RAHALEO ambaye ni MFANYA BIASHARA wa vyakula anayefanyia biashara yake Kibanda Maiti na anaishi mtaa wa RAHALEO alipofanyiwa unyanganyi huo. 
 Mfanya biashara huyu alifunga biashara yake majira ya saa 9:45 jioni ya siku hiyo ya tarehe 13/01/2014 na kuchukua pesa za mauzo ya kutwa jumla ya T.sh 11,500,000/= ambazo alizifunga katika bahasha /mfuko wa kaki na kuondoka nazo kuelekea nyumbani kwa kutumia gari yake no. Z. 128 EW NISSAN Rangi ya silver. 
Alipofika maeneo ya Raha Leo Kwa Mchina Tambi ndipo gari moja yenye no. Z.866 EX aina ya SCUDO ilipomzinga kwa mbele na ghafla aliona watu watatu wametokezea wakiwa na silaha mbili, moja ikiwa ni bastola na nyengine ni SMG. 
Watu hao walimlazimisha kwa usalama wake awape ule mfuko wenye pesa. Kwa kuhofia usalama wake alitoa pesa zote jumla ya T.SH 11,500,000/= Majambazi hao baada ya kitendo hicho cha kuchukua hizo pesa walikimbilia kwenye gari yao. 
Kitendo hicho kilifanyika mbele ya watu ambao walianza kupiga kelele za mwizi!, mwizi!, mwizi!, kelele ambazo zilimfanya dereva wa gari ya majambazi kuondosha gari na kuwaacha wenzao watatu chini. Wakati huo wananchi walipiga simu Polisi huku juhudi za ukamataji zikiendelea. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam akionesha bastola iliyotumia katika uhalifu wa kumpora fedha mfanyabiashara katika maeneo ya rahaleo Zanzibar ikiwa na risasi zake kamili, ilihusika katika tukio hilo.
 Kamanda Mkadam akionesha moja ya Silaha aina ya SMG ambayo ilikuwa haina magazine waliokuwa wakiitumia watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Raha Leo na kuitupa katika eneo la msikiti wa Muembe Shauri wakati wakikimbia.
Silaha zilizokamatwa na watuhumiwa wa ujambazi huo
Kamanda Mkadam akiwaonesha waandishi moja ya silaha aina ya Gobole,waliofanikiwa Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa wakati akijiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya mtoni.  
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam, kuhusiana na uhalifu uliofanyika mwanzo mwa wiki hii katika maeneo ya Rahaleo na kumpora fedha shilingi milioni kumi na moja katika tukio hilo na polisi kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, kwa ushirikiano wa Wananchi wa kwahani. Picha na Othman Mapara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kongole polisi kwa kuweza kufanikisha zoezi hili; natumai matukio mengine tunaweza kufanikisha hivi hivi; jengeni imani kwa wananchi na muwapende wananchi na si kuwanyanyasa. Wanannchi wanahitaji huduma na si kutukanwa, kunyanyaswa, n.k.

    ReplyDelete
  2. Tunawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa ushirikiano wao. Pia nawapongeza askari polisi kwa kuitikia mwitiko wa simu mara moja na kufika sehemu ya tukio. Hilo ndio linalotakiwa. Sio sehemu nyingine unapiga simu kwa polisi mpaka waje wafike baada ya masaa 3. Hiyo inakatisha tamaa wananchi na kutokuwa na imani na polisi wa mahali pale. Hongera sana

    ReplyDelete
  3. Je Afande Mkadam hapo umeshachukua "Fingerprint" maana naona unazikamata hizo silaha bila ya "Gloves"? Au ndio mambo ya "Forensic Evidence" hakuna TZ!!

    ReplyDelete
  4. mukadam ongezeni doria hasa maeneo yenye shughuli za biashara mm naamini unguja ni kisiwa kidogo mkijipanga maeneo ya mjini uhalifu utapungua

    ReplyDelete
  5. Hongera Bw Mukadam umeanza vyema.

    Endelea na moto huo wewe na wenzako na sisi tutakupa ushirikiano ili visiwa vyetu viwe na amani kama zamani.

    ReplyDelete
  6. Mbwa wa polisi tulioonyeshwa juzi humu walikuwa wapi hadi majambazi wapore kiasi kikubwa cha pesa?(Joke).

    Na hii ni changamoto kwa benki zetu.Wafanyabiashara wengi wanafunga biashara wakati benki nyingi zimefungwa.Kwa hiyo wafanyabiashara wana options mbili ama kuacha pesa ya mauzo madukani au kwenda nazo majumbani ili kesho yake wazipeleke benki.Njia zote hizi mbili ni hatari sana(very risk).ATM za kuweka(siyo kutoa tu) pesa 24hrs zinaweza kusaidia?maana zipo naziona huko "mamtoni" wanazitumia.

    David V

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 3 Finger prints zake Afande Mukadam zinajulikana hivyo hata zikichanganyika za mhalifu zitakuwepo tu ni vile zita tenganishwa na za huyo muhusika.

    Dunia ya sasa siyo ya kufanya Uhalifu ni vile Dijitali inakamata sana kila Idara!

    ReplyDelete
  8. Ile imani ya zamani na ule ubinaadam wa kuokota amana za watu zikapelekwa 'Sauti Ya Zanzibar' na kutangazwa muhusika akachukuwe amana yake haupo tena sasa hivi. Lakini kama walivyokwishachangia baadhi ya wadau hapo juu, nami naamini Unguja ni mithili ya 'Kijiwe' tu, naamini ulinzi ukiimarishwa vilivyo, usalam wa raia na mali zao, kuna uwezekano mandhari ikarejea kama zamani ya utulivu, amani na usalama. Mungu vibariki visiwa vyetu vya Unguja na Pemba.

    ReplyDelete
  9. Zanzibar mambo haya yalikuwa hakuna, hii ina maanisha polisi wawe macho kupambana vikali na uhalifu unaoongezeka ili wanaokamatwa wapelekwe mahakamani wafungwe ili iwe funzo kwa wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...