Taswira hizi ni sehemu ya nyumba za maeneo ya Temeke Wailesi jijini Dar es salaam ambazo zimeshapata namba katika mpango wa kuwa na Post Codes kwa jiji hilo kuu la biashara nchini Tanzania. Inasemekana asilimia 70 wakaazi wa jiji hilo wanaishi katika maeneo yasiyopimwa. Mpango huu uliozinduliwa Septemba 14, 2012 una lengo la kurahisisha taarifa ya makazi ya watu kwa mitaa kupewa majina rasmi na nyumba kuwekwa namba.
Home
Unlabelled
nyumba za dar es salaam zaanza kupewa namba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ujenzi holela umesababisha kukosa mitaa badala yake kuna vichochoro!!
ReplyDeletehata hivyo tuna jitahidi ina wezekana kila kitu polepole ndio mwendo hapo badomajina ya mitaa ikiwekwa itarahisisha baadhi ya mambo halafu basi muweke na ma tenki ya takataka.
ReplyDeleteNi mwanzo mzuri wa nyumba kuwa na Namba licha ya kuwa wanahitaji kuongeza Viashiria kama jinsi Serikali za Mitaa zilivyoweka Mfano MTONI KIJICHI unakuta namba ya nyumba ikiwa na Viashiria vya Herufi kama MTN/KJC/179 badala ya kuwa na Namba peke yake.
ReplyDeleteHata hivyo hii ni jitihada nzuri kuliko ilivyo kuwa kabla hata kumwelekeza mtu mfano mgeni inakuwa tabu!
Ni pale unatumia viashiria kama:
1.Ukifika Mbuyuni, nenda moja kwa moja, ukipinda kona utamwona Kinyozi chini ya mwembe kata kushoto niulizie pale duka la kwanza!
2.Ukitaka kufika kwangu, ukishuka Kituo cha basi, angalia upande wa kulia utaona uchochoro ukiufuata mwisho utata Maskani ya vijana, waulie watakufikisha kwangu.
Sasa hiyo siyo Mpangilio mzuri wa kuhitaji UFS (ama Mawakala wa Maulizo ili kufika sehemu)!!!