Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bw. Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu  akitoa maelezo ya utangulizi ya kufungua mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.
 Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro Mhe. Joel Bendera  akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.
 Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya Mgeni rasmi Mhe. Joel Bendera (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini.
 Juu na chini ni Baadhi ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Bene uliopo Morogoro mjini. Picha zote na Veronica Kazimoto
 Na Veronica Kazimoto – Morogoro
Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi popote pale duniani ni kigezo muhimu sana kinachotumika katika kupima na kufuatilia mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira ili kuiwezesha Serikali husika kuboresha Sera na Program mbalimbali za  kukuza ajira nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera wakati akifungua mafunzo ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa Bene mjini Morogoro.
“Utafiti huu mbali na kusaidia kufuatilia mwenendo wa soko la ajira nchini, husaidia pia kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Millennia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Malengo ya MKUKUTA”, amesema Bendera.
Bendera amefafanua kuwa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utatoa viashiria kama vile hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi, kiwango cha ukosefu wa ajira, kiwango cha ajira isiyo timilifu na ajira mbaya ambayo ni  hatarishi kwa watoto.
Viashiria vingine ni wigo wa hifadhi ya jamii na hali ya kipato kutokana na ajira, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2013. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifu ya Takwimu, amesema taarifa za hali ya soko la ajira zinazotumika kwa sasa bado ni zile za mwaka 2006.
“Takwimu za ajira zinazotumika sasa hazioneshi hali halisi ya mabadiliko yaliyotokea katika soko la ajira nchini, kutokana na hali hii Serikali pamoja na wadau wa maendeleo wameamua kufanya utafiti huu mwaka 2014 ili kupata hali halisi ya sasa”, amesisitiza Kwesigabo.
Jumla ya wadadisi na Wahariri 100 wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kutoka kanda ya Pwani na Kusini inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Mtwara na Lindi wanaendelea kupewa mafunzo juu ya Utafiti huo utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka huu.
Mafunzo kama haya yanafanyika katika kanda ya Ziwa, kanda ya Kati, kanda ya Kasikazini na kanda ya Juu Kusini ambapo ufunguzi rasmi umefanyika jana kwa baadhi ya kanda na leo katika maeneo mengine.

Mafunzo haya ya Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yanafanyika mara baada ya kukamilika kwa mafunzo ya Wakufunzi wa utafiti huo takribani wiki tatu zilizopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...