Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts 
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete,  wakiangalaia matumizi ya moja ya Tableti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 zilizotoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Go Cubs. Karibu Wriggleyville mheshimiwa.

    ReplyDelete
  2. michuzi naomba utoe habari kiuhalisia..je ni serikali ndio imenunua na inatoa hizi tablets au ni msaada wa huyo mmarekani?maana nijue kama mtoto wangu azisubiri kama ni za serikali au ni msaada wa huyo mmarekani kwa shule chache?

    baba Rama

    ReplyDelete
  3. Ohhh Jakaya Kikwete Basketball utaiweza?

    Naona hili fulana lililo andikwa nyuma 'PRESIDENT KIKWETE' ni kubwa sana yaani 'Puto' labda umkabidhi Ankal Michuzi mwenye Aleji ya kuvaa flana hata akivaa Suti!!!

    ReplyDelete
  4. Hahahaha Mdau wa 3,

    Hiyo nadhani ni kwa ukubwa wa maungo wa Wamarekani!

    Huku kwetu size hiyo ya fulana inakaribia kuwa sawa na Kanzu!

    ReplyDelete
  5. Hivi tabuleti ndio kiswahili cha tablet. Nchi jirani wanaita laptop kipakatilishi kwa kiswahili. Wataalam wa kiswahili changamkeni tupe neno la tablet(Kidonge?)..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...