Tarehe 21
Januari, 2014 Mhe. Begum K. Taj, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Hispania mwenye makazi yake Paris Ufaransa aliwasilisha Hati zake za
Utambulisho kwa Mtukufu Juan Carlos I,
Mfalme wa Hispania. Hafla hii ilifanyika kwenye kasri ya mfalme (Zarzuela
Palace) Madrid Hispania. Pichani Mhe. Balozi
Begum K. Taj akimkabidhi Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania, Hati zake za
Utambulisho.
Mhe. Balozi
Begum K. Taj pamoja na mabalozi wengine waliowasilisha hati zao wakimsikiliza
kwa makini Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania. Jumla ya Mabalozi 14
waliwasilisha hati zao siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...