Home
Unlabelled
Rais Kikwete aomba msaada kwa Serikali ya China kusaidia kupanga miji nchini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHivi kweli Tanzania hakuna wataalamu wa mipango mji? sitaki kuamini hili.
ReplyDeleteDuh inamaana hata wataalamu wa mipango miji hatuna ?sasa wizara iliyopo inajukumu gani?na kule kigamboni nilisikia kuna mji wa kisasa unajengwa hili nalo vp???
ReplyDeletetunao wataalamu wa mipango miji lakini uwezo wao ni mdogo lazima tukubali kusaidiwa. china si tanzania wako mbali na wameanza zamani mambo ya ujenzi.kuna mifano mingi tu.na misaada si pesa tu.
ReplyDeletetunao wataalamu wa mipango miji lakini uwezo wao ni mdogo lazima tukubali kusaidiwa. china si tanzania wako mbali na wameanza zamani mambo ya ujenzi.kuna mifano mingi tu.na misaada si pesa tu.
ReplyDeleteSasa hao wachina walisaidiwa na nani. Katika ulimwengu huu wa utandawazi na teknolojia bado tutaomba misaada ya kazi. kwahiyo wachina watupe hela, wajenge na sasa wapange. badala ya kuombwa wafanyakazi wako waendelezwe unomba ufanyiwe kazi. ukitaka kujenga Tanga nahiyo mikoa mipya inayozaliwa kila siku itakuaje? hivi sasa watu wana vyeti vya kuzaliwa kwenye mikoa isiyo yao tena... HII NI INCHI PEKEE DUNIANI INAYO JENGA MIKOA (KAMA NJIA YA AJIRA KWA WAKUU) NA KUOMBA KUFANYIWA KAZI. WAKATI WANANCHI HAWANA AJIRA...
ReplyDeleteWataalamu gani wadau hapo juu mnao dai tunao?, maana toka uhuru mpaka leo sijaona jipya la hao "so called wataalamu" Tatizo sio kusoma na kuwa na shahada, wataalamu wengi wana shahada lakini sio "creative" hupo hapo?
ReplyDeleteNakubaliana na mdau hapo juu.Uwezo wa wataalamu wetu ni mdogo. Hawana ubunifu, wengi hawajatoka wakaona miji ya wenzetu ilivyopangiliwa, wengi wamtoka kwenye nyumba zisizo za kisasa, wengi ni wababaishaji. Kuja kwa wachina sio tu ni faida ya nchi lakini pia inaweza kuwa fursa kwa wataalamu wa Tz kujifunza.
ReplyDeleteWaTZ tusiwe wepesi wa kulaumu kila kinachotendwa na serikali.
ReplyDeleteChuo cha ardhi hakikuanza leo, kipo miaka chungu nzima, na wataalamu hao waliomaliza chuo cha ardhi ndio waliopo serikalini kwenye mipango miji nk.
Lakini tunaendelea kuona miji mipya na viwanja vinatolewa bila kufikiria siku zijazo. hamna sehemu za mapumziko , viwanja vya watoto kuchezea maeneo ya shopping centres nk. Nafikiri tuwaachie wenye upeo waje kutusaidia.
natumai mtaniunga mkono
Mzee mmoja mstaafu katka fani ya mipango miji na ambae anaendelea kufanya kazi pale Ardhi University alipata kutuambia miaka zaidi ya kumi iliyopita kwamba hapa kwetu tatizo si kupanga ila tatizo ni kutekeleza! Alitueleza tukiwa wanafunzi wa fani isiyokuwa ya mipango miji kwamba tayari miji kadhaa ukiwamo wa Tanga ilikuwa na mipango mizuri ikiwamo na barabara za flyover zaidi ya miaka arobaini iliyopita. Tatizo kubwa ni utekelezaji katika mambo mengi sana hapa nchini naona wachina watakuwa tayari kupanga na kutekeleza walichopanga katika miji yetu kwa pesa zao na kuvuna tembo, gas uranium n.k
ReplyDeletesesophy
Nadhani wengi wetu mmeacha kitu kimoja, Wataalam wa Nchi hii wamezidiwa nguvu na wanasiasa, mimi ni shahidi wa wazi ktk hili mana nimefanya kazi ktk level za chini kabisa kama Halmashauri, utaona Madiwani/ Mameya/wenyeviti wa Halmashauri wanavolazimisha kuvunjwa kwa taratibu za mipango miji kwa manufaa binafsi ya kisiasa, mmesikia hata Magufuli alipokemea wavamizi wa barabra 'alikemewa' na Mamlaka za juu, so tusiwalaum wataalam bali politician wasioshaurika wala kufuata kanuni, pili kuomba msaada wa kitaalam sio dhambi hasa kwa miji kama yetu ambayo 'ishavurugwa' acha waje watusaidie kupangua ili kujipanga kimipango miji, asante
ReplyDeleteKuleta wataalamu kutoka nje siyo vibaya lakini kuwe na mkakati katika ziara yao kuwapatia watendaji wetu wa mikoa wilaya na makao makuu maelezo na nyenzo za teknolojia za kisasa kuimarisha utendaji wao, ili wanapoondoka wawezeshe watendaji wetu kwa kuimarisha taasisi zetu.
ReplyDeleteJamani naomba huu msaada wa kupanga miji iwe kwa nchi nzima sio tu Dar na vile vile naomba serikali iache kupasisha kila kitu Dar pelekeni na mikoani jamani ili watu wapate kazi na foleni zipungue maana kila biashara ,kampuni headquaretrs zinawekwa Dar mbona kwa nchi za wenzetu sio lazima endelezeni nchi nzima jamani
ReplyDelete