Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani sikukuu zote zinajulikana siku zake. Haya mambo ya kuamka na kutangaza siku kuu siku ambayo sio inashusha utendaji na maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  2. Tumerudi kulekule! Siku kuu J2 tunapumzika J3, au lengo ni kuwafurahisha Wazenj? Michuzi usibanie hii comment.

    ReplyDelete
  3. YAANI NIMEAMINI HIZI NI NCHI MBILI BUT DUGU MOJA KABISA, ZENJ OYEE

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 3 ni kweli kabisa!

    Ni muhimu pia kujua tuna undugu mkubwa na tumesha zaliana na kuchanganyika sana.

    Hivyo utengano ni vigumu na ukiona pana chokochoko uje pana maslahi kutoka nje na eno ama pana mwenye njaa zake hapo.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu juu,

    Huyo atakayeleta mabadiliko sema kupelekea mtu kutoka Zenj aje kwa visa bara ama wa bara aende kwa visa zenj, atakuwa ameleta mtafaruku mkubwa sana.

    Mfano upo bara mkeo na watoto wapo zenj umenyimwa visa kuingia zenj, inakuwaje?

    Mfano upo zenj unataka kuja bara umenyimwa visa kuja bara itakuwaje?,,,wakati maskani Bara Dar washikaji wamekuandalia chupa la Gongo na kete kadhaa za Majani, mwana zanzibari ukiwa Rasta kamili kweli utapata wasaa kumuenzi Bob Marley?

    Si itakuwa balaa juu ya balaa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...