Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Jaji Mstaafu
na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Damian
Zefrin Lubuva kufuatia kifo cha Mke wake, Mama Martha Peter Lubuva
kilichotokea tarehe 17 Januari, 2014 katika Hospitali ya Apollo iliyoko New
Delhi nchini India alikopelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa
wa Kisukari.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na
taarifa za kifo cha Mke wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa amelazwa
katika Hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa
Kisukari ambao umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais Kikwete
katika salamu zake za Rambirambi.
Rais Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi
sasa wanapitia watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin
Lubuva kutokana na kuondokewa na Mama yao Mzazi na Kiongozi
muhimu wa Familia, lakini amewaomba wawe watulivu na wavumilivu,
lakini muhimu zaidi wawe na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha
maombolezo ya mpendwa wao.
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba
huu mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na
kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva
kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola”.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014


.bmp)
Mwenyeez Mungu ampokee, amsamehe kwa yote na amlaze palipo pema peponi - AMEEN. Pole sana Mzee Lubuva pamoja na familia yako yote kwa jumla.
ReplyDeleteAmen. Sote tu wasafiri.
ReplyDelete