SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi linapita.
Hatua hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.
“Jana Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.
Alisema katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-. “Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.
Gharama hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani.
Punguzo ni sawa lakini mpejipanga kwa kuwa kuna watu wamelipia kuunganishiwa umeme tangu mwezi wa tisa mwaka jana hawajaunganishiwa. Mtanapopunguza gharama maana yake watu zaidi wataomba kuunganishiwa. Mmejiandaa na mafuriko hayo au mnaongeza nafasi za wafanyakazi wa Tanesco kupewa rushwa ili watu wawahishiwe kuunganishwa?
ReplyDeletesesophy
jamani watanzania tiwe na upe wa kifikiri zaidi yaani badala ya kupongeza kitendo kizuri cha punguzo mnaanza kufikiria rushwa kwa wafanyakazi. tuwe positive in thinking
DeleteLeo mmewapa upendeleo wa umeme kiasi cha bure....Nyumba za kufunga umeme je? wajengeeni pia....kesho watadai kupendelewa walipiwe mahari kuongeza wake......then watataka tena kupendelewa wapunguziwe nepi za watoto...! Msiwabebe sana kivile...!
ReplyDelete