Jumuiya ya Watanzania wa New York (ikijumuisha New Jersey, Connecticut na Pennsylvania) itafanya sherehe ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Jumapili tarehe 19 Januari 2014 kule Brooklyn. Anwani ya mahala sherehe itakapofanyika ni 3038 Atlantic Avenue, Brooklyn, NY 11208 kati ya Essex na Shepherd.

Watanzania na rafiki wa Watanzania wote mnakaribishwa. Kiingilio kitakuwa dola 15 kwa wakubwa na dola 10 kwa watoto. Kutakuwa na Vinywaji, chakula, mziki na mambo mengi mengine.

Vituo vya karibu vya treni J ni Norwood na Cleveland. Kumbuka Jumatatu ya tarehe 20 Januari 2014 ni Sikukuu ya Martin Luther King ambayo ni public holiday New York hivyo ni kusherehekea toka Jumapili hadi Jumatatu.

Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi Wasiliana nasi kupitia:

Email: info@nytanzaniancommunity.org
Simu: 201-252-7220, 917-557-3195

Wote mnakaribishwa.

Jumuiya ya Watanzania New York.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. New York wa Tanzania Community yenu ni ya sherehe tu. Hamna na mpango wa kuwasaidia watoto wenu wasome dini aibu hata Madrasaa hamna.Tution pia hamna. Watoto wenu watamjuaeje Mungu. Daa hatari wana Ndugu!!!!!

    ReplyDelete
  2. New York Tanzanian Community haina dini. Udini ni Nje ya community yetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...