Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) anatarajia
kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda
kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa
Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Kamati hiyo inayoundwa
na Maspika 37 walioteuliwa na Rais wa
Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye
Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge Duniani Mjini Geneva.
Mkutano wa pili wa Kamati
hiyo ya Maandalizi utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha,
kabla ya kwenda Geneva, Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika wa
Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika Wellington,
New Zealand kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2014.
Kwa
ujumla, ushiriki wa nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri ya
kuitangaza na kuipa heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa jukwaa
madhubuti linalotumika kuiweka nchi katika ramani ya dunia na kuonyesha vivutio
hususan katika nyanja za uwekezaji, utalii na maliasili pamoja na fursa
mbalimbali zilizomo.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
28 Januari 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...