Dear wadau, 
Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami. Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji.
Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa kama inavyoonesha hapa:
Ujumbe huo unasomeka kama hivi:
TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku
Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa
kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi.
Asante tena kwa ushirikiano wako,
Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dear wadau, taarifa sahii, Upotishaji ... kuweni makini kwenye kazi jamani, loh!

    ReplyDelete
  2. MAMLAKA YA HALI YA HEWA JITAZAMENI NA MUONE KAMA HIZO TAARIFA SAHIHI MNAZOZITOA KAMA ZIKO KWENYE VIWANGO AU MNATIMIZA WAJIBU WA WA AJIRA. UKWELI TAARIFA ZENU ZIKO KWENYE VIWANGO VYA CHINI SANA KIASI VINATUFANY TUZIPUUZE TAARIFA ZENU AMBAZO MARA NYINGI HUWA ZA JUMLAJUMLA NA WAKATI MWINGINE HUWA ZIMEPITWA NA WAKATI. UPEPO UNAOVUMA DAR ES SALAAM SASA SI UPEPO WA TAHADHARI KWANI HAUNA TOFAUTI NA UVUMAO MAKAMBAKO AU SINGIDA HATA SAME. HIVI ILE RADA MLIYOSEMA ITABORESHA UTABIRI NA IKATULIA MAPESA MPAKA WAINGEREZA WAKATUONEA HURUMA WATOTO WAKE TUKAREJESHEWA CHENJI ILIISHIA WAPI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...