Katika kipindi cha sikukuu ya
Mwaka mpya Mkoani Dodoma yamejiri matukio kadhaa.
Katika tukio la pili, mnamo
tarehe 31/02/2013 saa 20:00hrs usiku katika kijiji cha Ndalibo Kata ya Mtanana
Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma.
Mtu aliyefahamika kwa jina la KAMOTA s/o CHIMASI,
50yrs, Mkagulu, Mkulima na mfugaji, mkazi wa Ndalibo, aliuwawa kwa kupigwa
risasi mgongoni kwa kutumia bunduki aina ya Gobore na watu wasiofahamika wakati
akiwa nje ya zizi akihesabu ng’ombe wake. Katika tukio hilo hakuna kilichoibiwa
na Chanzo mauaji hayo bado hakijafahamika.
Watu watatu wanashikiliwa na Polisi
kwa mahojiano pamoja bunduki aina ya gobore na Upelelezi unaendelea kubaini chanzo na sababu ya tukio hilo.
Katika tukio la tatu, mnamo
tarehe 01/01/2014 majiraya saa 01:00hrs usiku huko eneo la barabara ya 11 Kata
ya Madukani Manispaa ya Dodoma, duka la vifaa vya Kielectronic linalomikiwa na
MARRY d/o RICHARD, 32yrs, Mchaga, Mfanyabiashara mkazi wa Nkuhungu Dodoma
lilivunjwa na mali mbalimbali zikiwemo simu 150, digital camera 6, redio Sub
–hoofer 7 na pasi 5 vyote vikiwa na thamani ya Tsh. 7,665,000/=.
Mbinu
iliyotumika ni kuvunja kwa kukata Seilingbaord kutokea upanda wa nyumba ya kulala
wageni iitwayo NASIBU chumba namba 2 na kutokeza dukani kwa kuwa duka hilo
limeungana na nyumba ya wageni. Hakuna mtu aliyekamatwa na upelelezi wa tukio
unaendelea.
Katika tukio la nne mnamo
tarehe 01/01/2014 majira ya saa 12:00hrs mchana katika kitongoji cha Mhuti
kijiji cha Chigongwe Manispaa ya Dodoma. Bibi kizee aliyefahamika kwa jina la
EMMY d/o MJENZI @ MCHIMBU, 106yrs, mgogo, Mkazi wa Mtaa wa Mhuti kijiji cha
Chigongwe, alifariki dunia kwa kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya
mbuyu iliyosokotwa. Marehemu huyo aliwahi kujaribu kujinyonga mara mbili mwezi
Mai,2013 na mwezi Novemba, 2013 lakini aliokolewa. Sababu ya kujinyonga ni
kuchoka kuishi kwa muda mrefu. Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.
Tukio la tano mnamo tarehe 31/12/2013
Mjaira ya 21:00hrs Katika mtaa wa Mbabala “A” kijiji cha Mbabala Manispaa ya Dodoma,
mtoto aliyefahamika kwa jina la IRENE d/o SIMPHORIAN, 7yrs, mgogo, mwanafunzi darasa
la kwanza S/Msingi Mwenge, alipotea katika mazingira ya kutatanisha nyumbani
kwake baada ya kuachwa pekeyake na wazazi.
Alipatikana mnamo tarehe 01/01/2014
saa 17:00hrs akiwa amefariki dunia eneo la pori la jirani umbali mita 300 kutoka
nyumbani kwaopia ni jirani na Kanisa la Anglikana. Hakuna mtu aliyekamatwa
kuhusiana na tukio hilo, uchunguzi wa mwili wa marehemu unafanyika na upelelezi
zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.
Jeshi la Polisi linaendelea
kusisitiza wananchi wake kutojichukulia sheria mkononi na badala yake watoe
taarifa Polisi mapema ili kuokoa uhai wa watu na malizao. Aidha wafanyabiashara
wahakikishe mali zao zinakuwa katika mazingira salama na kutoruhusu mianya kwa
wahalifu kuvunja na kuiba.
SUZAN
KAGANDA -ACP
KNY:
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...