MWEKA Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mchezaji wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo TASWA Fc,  Sultan Sikilo (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitli ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kufuatia maladhi ya Homa ya Ini yaliyokuwa yakimsumbua.

Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa TASWA, Amir Mhando amesema kuwa, Sikilo alifikishwa hospitalini hapo  ambako umauti umemfika akitokea hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, Alhamisi ya wiki hii.


“Ndugu yetu aligundulika ana matatizo ya homa ya ini siku ya Alhamisi katika hospitali ya Temeke na akahamishiwa Muhimbili, ambako umauti umemfika,”amesema Mhando.

Aidha, Mhando amesema kuwa msiba wa marehemu Sultan upo nyumbani kwa wazazi wake Mbagala Maji Matitu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Saa 9:00 Alasiri eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ua marehemu Sultan mahali pema peponi. Amin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...