Katika kukabiliana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea kushika kasi ndani nan je ya mipaka ya nchi yetu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litaendeshwa katika mfumo wa jeshi-usu katika siku chache zijazo ambapo watumishi wake watalazimika kupitia katika mafunzo maalum ya kijeshi.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya askari wapya 96 walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi minne katika Hifadhi ya Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.

Kijazi alisema kuwa TANAPA imeanzisha utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka katika Vyuo vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na shirika kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya utendaji kazi katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiongea kabla ya kufunga rasmi mafunzo hayo.
Wahitimu wakionyesha igizo la namna ujangili unavyoendelea na mbinu za askari katika kukabiliana na vitendo hivyo vya ujangili katika maeneo ya hifadhi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HUU NI UAMUZI MZURI NA UNAHITAJI PIA KUHARAKISHWA NA UTENDAJI WAKE USIMAMIWE VIZURI ILI KUEPUKA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA AWALI ZA MSUGUANO NA WANANCHI WANAOISHI JIRANI NA MAENEO YA HIFADHI. VILE VILE HIFADHI ZA BAHARI ZIUNGANISHWE NA TANAPA MAANA ZIPO ZIPO TU KAMA YATIMA VILE, UTENDAJI WAKE KWA KWELI UNASUA-SUA SANA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...