Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja
ya Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni
Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw. John Mayopa
na anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.
Mmmoja wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester
Mganga akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya
kazi. Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini aina ya ‘dimension stone’ na
kokoto za ujenzi katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo.
Mwakilishi wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli
akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo
kuhusu Kampuni hiyo. Leseni iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha
kuchimba madini ya Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.
Mwakilishi wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao
cha kusaini Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya
kuchimba madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.
Na Asteria Muhozya
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo ameweka saini
Leseni tatu za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha
madini aina mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli
hizo.
Kampuni zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction,
inayomilikiwa na Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw.
Nakui Chen Kampuni hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa
wa km 0.29. Aidha, shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la
Kihangaiko Bagamoyo na Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’
na kokoto za ujenzi za granite.
Vilevile, kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T)
Ltd. inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni
namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu
katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita.
Aidha, Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina
ya Marble kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari
ambao wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa.
Kampuni hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.
Wakati akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa
leseni kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili
wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo
umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.
muheshimiwa ndugu waziri ni lini utatia saini uchimbaji wa urani(mkuju river project)
ReplyDelete