Na Abdulaziz Video,Lindi
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)mkoani Lindi,limeanza kupokea vifaa
mbalimbali,zikiwemo nguzo,Mita na waya,vitakavyotumika kuwaunganishia
wateja wapya wapatao 1,413 waliokwishaomba kupatiwa huduma hiyo na
kulipia kati ya June na Disemba 2013.
Meneja wa Shirika hilo mkoani Lindi,Eng John Bandiye ameyaeleza hayo
jana alipokuwa akizungumza na timu ya waandishi wa Habari kuhusiana
na jitihada za shirika kutoa huduma kwa wateja.
Vifaa hivyo vimeanza kuwasili mkoani hapa,kuanzia mwanzoni mwa mwezi
huu, na tayari vimeanza kugaiwa Katika wilaya zote tano zilizopo
katika mkoa huo.
Amevitaja vifaa vilivyowasili kuwa ni pamoja na Mita za LUKU 1,413,
Nguzo 450 kwa ajili ya Service Line katika njia kubwa za umeme na
kwenye mita majumbani.
Meneja Bandiye amefafanua kuwa kufuatia kupatikana kwa vifaa
hivyo,tayari wateja wapatao 1,413 waliotuma maombi ya kupatiwa umeme
na kulipia kwa muda mrefu uliopita ,wataunganishiwa huduma hiyo katika
kipindi kifupi kijacho kuanzia sasa,ili waondokane na tatizo hilo
lililodumu kwao kwa muda mrefu.
Aidha ameeleza pia katika maombi 1,413 waliyoyapokea kutoka kwa
wateja wapya mwaka 2013,wapo 1,132 hawahitaji nguzo na 281 ndio
wanaohitaji kupelekewa nguzo na kubainisha kwa kusema wilaya ya Lindi
waliotuma maombi yao ni (509) kati ya hao (73) wanaohitaji kupelekewa
nguzo,Nachingwea 322 wasiohitaji nguzo ni 263,Kilwa 275 wakiwemo (81)
wanaohitaji nguzo,Liwale 154 kati yao 128 hawahitaji nguzo na Ruangwa
wapo 153 wanaohitaji huduma ya nguzo ni 42.
"Tatizo kubwa lililochelewesha wateja wetu wakae muda mrefu ilikuwa ni
vifaa,kwa vile vimewasili tatizo hilo,naweza kusema limeisha na kazi
ya kuwaunganishia wateja wetu limeanza,hivyo hadi kufikia mwishoni mwa
mwezi Februari 2014,zoezi la kuwaunganishia umeme liwe limekamilika"
Alisema Bandiye.
Kutokana na kufika kwa vifaa hivyo amewashauri wale wateja wapya ambao
walikuwa wakisita kulipia kwa hofu ya kuchelewa kuunganishiwa,wafanye
hivyo bila ya kukosa ili na wao waweze kufungiwa Mita kwa lengo la
kupatiwa huduma waliyoiomba ambayo pia kwa sasa imepunguzwa bei hadi
kufikia 27000 kwa wateja walio vijijini kulikopita bomba la Gesi
Meneja wa Tanesco mkoa wa Lindi Eng John Bandiye
Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Lindi.
baadhi ya Vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kuondoa
kero za umeme ikiwa ni pamoja na kuondoa ukatikaji wa umeme mara kwa mara
kwa sababu ya Nguzo kuchakaa na kuanguka mara kwa mara hususan katika
njia kuu ya Mtwara.
Hi Uncle,
ReplyDeleteSiku nyingine edit uondoe huyo jamaa aliyevaa mlegezo ktk picha ya watu wanaovuta nguzo
Observer