Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za Tuzo za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo ya Singida, Fidel Samwel mmoja wa washindi wawili wa jumla wa shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Fidel pamoja na mwenzake Jafari Ngadula wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za Tuzo za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...