Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Martha Qorro akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara (wa kwanza aliyekaa kulia) kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa mara alipozindua Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa Bw. Selemani Hegga akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa Bodi hiyo hawapo( pichani) katika shughuli ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akipata maelezo mafupi kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza kuhusu Ukumbi wa ndani wa Maonyesho wa Sanaa alipotembelea BASATA leo jijini Dar es Salaam (jana), watatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleao ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akitoa maelekezo kwa Wadau wa Sanaa alipotembelea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kujionea shughuli zinazofanywa na Baraza hilo,nyuma ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waziri Finella, asante sana kwa huo mtindo wa nywele!

    ReplyDelete
  2. Mh. Waziri, I really like your 'personality',you always look so simple and smart. Huna ku-complicate muonekano wako. Kadhalika katika suala zima la majukumu na uwajibikaji wako, unastahili pongezi.

    ReplyDelete
  3. Namkubali sana waziri huyu kwa staili yake. Napenda sana mama na dada zetu wangekubali jinsi walivyo kwamba waafrika yani tungeishi vizuri sana bila shida. Hongera sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...