Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite. 

Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. 

Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.
Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.
Mtaalamu wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani Bw. Damian Mansala akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kupeleka wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini uliochimbwa na kuusambaza katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Tanzanite.
Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza ujumbe wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya kumaliza ziara Mkoani humo.
Meneja Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali (mwenye kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kusafisha na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hayo masalia ya flamingo ni vivutio vya kitalii vikitangazwa na vitadumu milele, lakini cha ajabu tunauza na kukimaliza bila huruma kwa njaa ya siku mbili badala ya kuwa kipato cha milele. Hivi sisi watu weusi tuna nini? Mbona tunajikaanga wenyewe na kuweka wazu uwezo wetu wa kufikiri.Inauma sana, serikali inabidi iwe ya akili ya kuona kipi ni utalii na kipi kiliwe. Nawakilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...