Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko akiongea na Ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina na maadhimisho ya Miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho, mgeni rasmi atakuwa Mhe.Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko akisikiliza jambo kutoka kwa Mshauri wa Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Nchini Liu Dong wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake juu ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina na maadhimisho ya Miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof: Hermas Mwansoko (Kulia) akipokea Kitabu chenye Historia ya Mchezo wa Karate kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa Mchezo huo Shi yan Cen (Kushoto) ikiwa ni ishara ya kuendelea kudumisha ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na China.(Picha zote na Benjamin Sawe wa Wizara ya Habari).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...